Mpanda FM

Bei ya mafuta yapaa wananchi walalamikia ugumu wa maisha Mpanda

6 November 2026, 2:12 pm

Picha ya mafuta . Picha na mtandao

“tunashindwa hata kwenda vijiji vya jirani kufuata mazao bei ya nauli imekua kubwa hakuna faida“

Na. Leah Kamala

Wananchi mkoani Katavi wameiomba serikali kuangalia upya kupanda kwa bei ya mafuta nchini, kutokana na kuongezeka kwa gharama za maisha katika sekta ya usafirishaji.

Wakizungumza na mpanda radio fm, kwa nyakati tofauti wananchi hao wameeleza kuwa kupanda kwa bei ya mafuta kumeweza kuchochea ongezeko la nauli na kufumuka kwa bei za bidhaa mbalimbali.

Sauti ya wananchi

Wakati wananchi wakielezea changamoto hizo, mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetangaza ongezeko la bei kikomo za mafuta kwa mwezi November 2026 ambapo kwa Mpanda bei ya mafuta ya petrol ikiuzwa shilingi 4301, dizeli ikiuzwa shilingi 4346, na mafuta ya taa yakiuzwa shilingi 4335.

Wilaya ya  Mlele bei ya mafuta ya petrol ikiuzwa shilingi 4283, dizeli ikiuzwa shilingi 4328, na mafuta ya taa yakiuzwa shilingi 4317, Mpimbwebei ya mafuta ya petrol ikiuzwa shilingi 4320, dizeli ikiuzwa shilingi 4365, mafuta ya taa yakiuzwa 4354 na Tanganyika bei ya mafuta ya petrol ikiuzwa shilingi 4319, dizeli ikiuzwa shilingi 4364, huku bei ya mafuta ya taa yakiuzwa shilingi 4353.

Katika mwezi October 2026, bei za mafuta yaliyosafirishwa katika soko la dunia zilipungua kidogo ukilinganishwa na mwezi Septemba lakini bado ziliendelea kuwa juu. Hata hivyo, kuendelea kwa mgogoro wa mashariki ya kati, ambako Tanzania hununua sehemu kubwa ya mafuta yake, kumeongeza gharama za usafirishaji na bima, hivyo bei za petrol, dizeli na mafuta ya taa nchini zimeongezeka katika mwezi November 2026, ikilinganishwa na October 2026.

Ili kukabiliana na athari hizi, serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa soko la dunia na kuchukua hatua za kuhakikisha upatikananaji wa uhakika wa bidhaa za mafuta na kuwapunguzia wananchi makali ya bei.