Mpanda FM

Chanjo za watoto ni kinga dhidi ya ulemavu unaoepukika

4 November 2026, 12:58 pm

Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa katavi Daktari Paulo Kilenga. Picha na Leah Kamala

“tusipuuze chanjo tangu kipindi cha ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka 2“

Na. Leah Kamala

Wazazi na walezi mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia ratiba ya chanjo kwa watoto  ili kuwakinga na magonjwa yanayoweza kusababisha ulemavu pamoja na madhara ya kiafya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mpanda radio fm, wazazi hao wamesema kuwa kuwapeleka watoto kupata chanjo ni wajibu wa kila mzazi ili kusaidia kulinda afya za watoto na kupunguza hatari ya kusambaa kwa magonjwa katika jamii

Sauti ya wazazi

Nae daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa katavi Daktari Paulo Kilenga amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote zinazohitajika na kuwahi katika vituo vya afya kwa ushauri Zaidi.

Sauti ya daktari Kilenga

Aidha daktari kilenga ametoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto chanjo tangu wanapozaliwa, pia waepukane na Imani potofu dhidi ya chanjo.

Sauti ya daktari Kilenga 2

Wazazi na walezi wanahimizwa kushirikiana na wataalamu wa afya kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo kwa wakati, hatua itakayosaidia kulinda afya ya mtoto na jamii kwa ujumla.