Mpanda FM

Mwanaume afariki dunia kwa kunywa sumu Mpanda

24 November 2026, 12:41 pm

Picha ya mfano wa sumu. picha na akili unde

“wanaume msikae na changamoto zenu jaribuni kuwashirikisha watu wa karibuau wazee“

Na. Mwandishi wetu

Anthony Juma, mwenye umri wa miaka 34, mkazi wa Mtaa wa Tulieni, Kata ya Nsemulwa, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa sumu

Wakizungumza na vyombo vya habari ndugu wameeleza kusikitishwa na tukio hilo huku  wakibainisha  kutofahamu Chanzo cha tukio hilo.

Sauti za ndugu wa marehemu

Kwa upande wao baadhi ya majirani wameeleza kuwa siku ya tukio marehemu  alichelewa kuamka tofauti na siku nyingine na walipoenda nyumbani kwake walikuta mlango umefungwa na msumari na viti vikiwa vimepangwa juu ya mlango.

Sauti za majirani

Kwa upande wa viongozi wa serikali mtaa wa Tulieni wameeleza kuwa na taarifa ya tukio hilo na hatua zilizochukuliwa ambapo wamewataka wananchi kuepuka kukaa na changamoto zinazowakabili na kuwashirikisha viongozi wa dini na watu wanaowaamini.

Sauti za viongozi wa serikali ya mtaa