Mpanda FM
Mpanda FM
8 October 2026, 10:01 am

“Kila kaya itachangia shilingi elfu nane“
Na. Ben Gadau
Wananchi wa eneo la Kilimahewa magomeni, Mtaa wa Kasimba wameanza kuchangishana fedha kwa ajili ya ujenzi wa kivuko kilichopo eneo hilo wakisema ni hatua inayolenga kupunguza changamoto kwa wananchi kuvuka wakati wa mvua zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza Mwenyekiti wa Mtaa wa Kasimba, Bernad Nswima, amesema wananchi wameamua kuchukua hatua mapema kwa kujenga kivuko hicho ili kuepuka usumbufu na hatari zinazoweza kujitokeza pindi mvua zitakapoanza kunyesha.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi wa mtaa huo wamesema kuwa wamekubaliana kuchangishana shilingi elfu 8 kila mwananchi ili kujenga kivuko hicho ambacho wamesema kuwa kimekuwa kikwazo hasa kipindi cha masika.