Mpanda FM

Wawili wapoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi Mpanda

23 October 2026, 10:28 am

Kibao cha eneo la uchimbaji wa madini. Picha na Restuta Nyondo

“kuanagalia pale tukakuta aliyebondwa mmoja anaonekana kichwa ilamwingine alikua haonekani kabisa“

Na.Ben Gadau

Watu wawili ambao majina yao bado hayajafahamika wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi katika migodi iliyopo katika kijiji cha Kapanda, halmashauri ya wilaya ya Nsimbo, mkoani Katavi.

Akizungumza kwa njia ya simu leo oktoba 21 katika kipindi cha kumekucha Tanzania, mwenyekiti wa kijiji cha Kapanda, John Gwanchele Mpemba, amesema kuwa vifo hivyo vimetokea usiku wa kuamkia Oktoba 20, mwaka huu, baada ya watu hao kuingia mgodini usiku na kuanza shughuli za uchimbaji, kabla ya kukumbwa na maafa hayo.

Sauti ya mwenyekiti

Mwenyekiti huyo amewataka wachimbaji kuchukua tahadhari na kuzingatia usalama wanapokuwa migodini, hususani katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa mvua za masika, ambazo zinaweza kuongeza hatari ya kuanguka kwa vifusi na kusababisha vifo kwa wachimbaji.

Sauti ya Mwenyekiti 2