Mpanda FM
Mpanda FM
25 November 2026, 7:38 pm

“ukatili wa kingono dhidi ya wasichana unaotokana na mila na desturi zenye madhara bado ni changamoto mkoani hapa“
Na. Restuta Nyondo
Ukatili wa kingono unaochochewa na imani za kishirikina na mila na desturi zenye madhara umetajwa kuwa bado ni changamoto mkoani Katavi.
Akizungumza katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na jeshi la polisi Katavi afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi Anna Shumbi amesema kuwa bado aina mbali mbali za ukatili ni kikwazo hususani ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na Watoto wakiwa wahanga zaidi kuliko wanaume.
Kamishna msaidizi wa polisi ACP Haji Mohameid mgeni rasmi aliyemuwakilisha Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi amesema kuwa jamii inapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa na kushiriki katika kuzuia vitendo vya ukatili na kuwataka wenyeviti wa wa serikali za mitaa na vijiji kuacha kumaliza kesi hizo mtaani ili kutokomeza ukatili miongoni mwa jamii.
Uzinduzi huo umehusisha jeshi la polisi,maafisa ustawi na maendeleo ya jamii,viongozi wa dini wananchi na asasi zisizo za kiserikali zinahusika na kupinga ukatili.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huanza tarehe 25 November hadi 10 December na Tanzania yanaongozwa na kauli mbiu isemayo tuungane kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto Jenga Taifa imara lenye haki na usawa kuelekea Dira 2050.
