Mpanda FM
Mpanda FM
30 October 2026, 11:20 am

“punde kidogo tukaona bati inanyanyuka tukatoka tunakimbia “
Na. Ben Gadau
Zaidi ya nyumba 20 zimeathiriwa na mvua zilizonyesha na kuambatana na upepo mkali katika kata ya Nsemulwa, hususani katika mitaa ya Migazini na Kasimba, mkoani Katavi.
Baadhi ya nyumba zimeezuliwa paa na nyingine kuanguka, huku wakazi walioathirika wakiomba msaada kutoka serikalini na kamati za maafa ili kukabiliana na hali hiyo.
Akitoa taarifa kuhusu athari hizo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Migazini, Kennedy Kaobwe, amesema nyumba tisa zimeathirika baada ya upepo mkali kuondoa mabati na kuezua sehemu za paa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kasimba amesema nyumba 17 zimeezuliwa paa na mabati, huku watu wawili wakijeruhiwa kutokana na mvua hizo.
Kwa mjibu wa tarifa iliyotolewa na Manispaa ya Mpanda imetaja maeneo mengine yaliyoathirika ni kata ya Kasokola, Uwanja wa ndege, Shanwe na Ilembo ambapo takribani nyumba 25, ikiwa ni pamoja makazi ya wananchi, madarasa, nyumba za ibada na vyoo, zimeezuliwa paa, huku baadhi ya majengo yakiwa na kuta zilizoanguka. Hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kukabiliwa na changamoto ya makazi.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari wanapoona dalili za mvua kubwa na upepo mkali kwa kukimbilia maeneo salama pamoja na familia zao ili kuzuia madhara zaidi.