Mpanda FM

Wananchi kuweni na utaratibu wa kupima afya

17 November 2026, 1:51 pm

Daktari Salvius Ngahyolerwa, daktari bingwa kitengo cha matunzo na tiba kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi. Picha na Leah Kamala

“Serikali iongeze juhudi katika utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupima afya mara kwa mara“

Na. Leah Kamala

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kujenga utaratibu wa kupima afya zao ili kubaini uwepo wa magonjwa mbalimbali na kupata matibabu kwa wakati.

Wakizungumza na Mpanda radio, wananchi hao wameeleza kuwa bado kuna haja ya kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya ili kutambua magonjwa yanayowasumbua.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wake daktari bingwa kitengo cha matunzo na tiba kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi daktari Salvius Nyahyolerwa amesema kuwa kupima afya kunasaidia kugundua magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kupunguza uwezekano wa kupata madhara makubwa ya kiafya.

Sauti ya Daktari 1

Aidha daktari Salvius ameelezea madhara ya kutopima afya mara kwa mara kunaweza kusababisha magonjwa kugundulika hatua za mwishoni hivyo kuongeza changamoto za matibabu.

Sauti ya Daktari 2

Wananchi mkoani Katavi wanahimizwa kuachana na dhana potofu ya kupima afya pale wanapougua badala yake wafanye uchunguzi mapema ili kupatiwa matibabu.