Mpanda FM
Mpanda FM
7 October 2026, 5:54 pm

“wakulima watalima zaidi ya mara moja“
Na. Betord Chove
Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, amesema ujenzi wa bwawa katika Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji Mwamkulu utachochea uzalishaji wa mazao na kuwawezesha wakulima kufanya kilimo zaidi ya mara mbili kwa mwaka.
Chongolo amesema ili kuendelea kufanya kilimo kiwe na tija mkoani Katavi, Serikali imepokea maombi na mapendekezo ya viongozi wa mkoa huo ikiwemo ombi la bwawa hilo, ombi la kuongeza msukumo wa pembejeo kwa wakulima, miundombinu na kupanua soko la mazao kwa kuongeza thamani ya mazao.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameiomba Serikali kuendelea kuhakikisha miundombinu na pembejeo za wakulima zinakuja kwa wakati ili kuweka hamasa kwa wananchi kuzalishaji wa mazao ya kimkakati ya tumbaku, alizeti, pamba, mahindi na mpunga
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa mitano inayotegemewa kwa kilimo nchini Tanzania. Asilimia 90 ya pato la mkoa linategemea shughuli za Killimo.