Mpanda FM
Mpanda FM
30 October 2026, 1:03 pm

“vijana wengi wanapata magonjwa kama saratani ya koo na changamoto za afya ya akili kwasababu ya matumizi ya vilevi“
Na. Leah Kamala
Wananchi mkoani Katavi wameiomba serikali na wadau wengine kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ili kuwasaidia vijana kuepukana na matumizi ya dawa hizo.
Wakizungumza na mpanda radio fm, wananchi hao wamezungumzia sababu mbalimbali zinazopelekea vijana wengi kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya
Kwa upande wake Daktari bingwa wa afya ya akili na magonjwa ya akili kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi Edward Bucheye amesema matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kusababisha matatizo ya kiakili na kimwili hivyo ni vyema waathirika wakapatiwa matibabu badala ya kuwanyanyapaa.
Kupitia taarifa iliyotolewa tarehe 29sept.2026 na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na dawa za kulevya (DCEA) Aretas Lyimo amesema mamlaka ilikamata jumla ya kilogram 18,078.41 za dawa za kulevya nchini katika kipindi cha julai hadi septemba 2026
.