Mpanda FM

Katavi Hippos marathon yatoa bima kwa watoto 20 wenye ulemavu

10 November 2026, 7:22 pm

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akimkabidhi mtoto bima ya afya. Picha na John Benjamin

“Marathon hii iwe mfano kwa wengine kwani bado kwenye jamii wapo wengi wasiojiweza wanaweza kusaidiwa kupitia michezo”

Na. John Benjamini

Jumla ya watoto 20 wenye mahitaji maalumu wamepatiwa Bima za afya kupitia mbio za Katavi Hippos Marathon iliyofanyika katika uwanja wa Ccm Azimio wilayani Mpanda mkoani Katavi

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusufu amempongeza mwaandaji wa mbio hizo kwa kubuni na kujitolea kuwapatia mchango huo huku akimtaka mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda kuwa na utaratibu wa mara kwa mara watu kufanya mazoezi na kushiriki michezo kwa pamoja.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

Kwa upande wake Beletia Wiliam Kafipa mkurugenzi wa Taasisi ya Mama Afrika Tanzania Vision Sport Academy wakiwa ndiyo waandaji wa mbio hizo za Katavi Hippos Marathon amesema kuwa mbio hizo kwa mwaka huu zilikuwa na nia ya kurudisha kwa jamii ambapo imefanikiwa kuwafikia watoto 20 kwa kuwapatia bima za afya.

Sauti ya Mama Afrika

Mohamed Katoto afisa uanachama mwandamizi NHIF Katavi amemshukuru mwaandaji wa mbio hizo kwani zaidi ya shilingi Milioni Moja imetumika kuwapatia bima hizo ambazo watatumia kwa mwaka mmoja huku akisisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kukata bima ya afya kwa wote ambayo ni agizo la Rais la kila mwananchi kupata bima ya afya kwa wote.

Sauti ya afisa uanachama NHIF

Kwa upande wao baadhi ya washiriki waliojitokeza kushiriki mbio hizo wamesema kuwa ni hatua nzuri iliyofikiwa ya kuwakumbuka baadhi ya watoto wenye mahitaji maalum na kuhakikisha wanapata tabasamu

Sauti ya washiriki wa marathon

Mbio za Katavi Hippos Marathon zimehudhuriwa na makundi mbali mbali ambapo wakimbiaji wamekimbia kilometa 5 na kilometa 10.