Mpanda FM

TAKUKURU yaokoa zaidi ya milioni 500 fedha za mikopo ya 10% ya halmashauri

30 October 2026, 12:50 pm

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Katavi Sipha Mwajala akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Marco

“kuna fedha zimerejeshwa baada ya kufanya ufujaji wa malipo “

Na. Betord Chove

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 591.2 katika kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026, zikiwemo shilingi milioni 229 zilizokuwa zimekopwa na vikundi mbalimbali kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Sipha Mwanjala, amesema mafanikio hayo yametokana na hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Sauti ya mkuu wa Takukuru Katavi

Ameiomba jamii kuendelea kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za viashiria vya vitendo vya rushwa, hususan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ili hatua stahiki zichukuliwe na kulinda rasilimali za umma

Sauti ya mkuu wa Takukuru Katavi 2