Mpanda FM
Mpanda FM
23 October 2026, 11:01 am

“washirikiane na ofisi ya taifa ya takwimu kutoa tarifa sahihi ili kusaidia kupanga masuala ya kiuchumi“
Na. Leah Kamala
Wananchi mkoani Katavi wametoa maoni yao kuhusu takwimu huku wakiiomba serikali kuendelea kutoa elimu ili kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa takwimu katika kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Wakizungumza na mpanda radio fm, katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani, ambayo huadhimishwa kila tarehe 20/10 wananchi hao wamesema kuwa elimu hiyo itasaidia katika ukusanyaji wa takwimu.
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa kitengo cha mahusiano kwa umma na mawasiliano, ofisi ya taifa ya takwimu (NBS) Benton Nollo amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu takwimu katika maendeleo ya taifa.
Aidha Nollo amewahimiza wananchi kutoa ushirikiano kwa ofisi ya taifa ya takwimu ili kuwezesha upatikanaji wa takwimu zenye ubora zitakazosaidia serikali kuweka mipango ya kuboresha maisha ya watanzania.
Siku ya takwimu duniani inaangazia mchango wa takwimu katika kufanya maamuzi sahihi, kupanga sera na kufatilia maendeleo.