Mpanda FM

Mgawanyo sawa wa majukumu msingi wa kujenga familia kiuchumi

4 November 2026, 12:35 pm

Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda Anyulumye Longo. Picha na Leah Kamala

“ili kujenga familia yenye ustawi endelevu ni muhimu kushirikiana na kujenga familia imara“

Na. Leah Kamala

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia umuhimu wa kugawana majukumu ya familia ili kupunguza mzigo wa kazi na kuimarisha amani, na upendo katika familia.

Wakizungumza na Mpanda radio fm, wananchi hao wameeleza kuwa majukumu ya familia yanapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano na kushiriki katika shughuli za kiuchumi za familia

Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Anyulumye Longo amezungumzia umuhimu wa kugawana majukumu ya familia, ili kusaidia kupunguza migogoro na kuleta maendeleo katika familia.

Sauti ya afisa ustawi

Aidha Longo ametoa wito kwa familia kushikamana ili kufanya maamuzi kwa pamoja katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Sauti ya afisa ustawi 2

Mgawanyo wa majukumu ni muhimu katika kujenga upendo, mshikamano na amani miongoni mwa wanafamilia ili kuimarisha mahusiano mazuri ndani ya familia.