Mpanda FM
Mpanda FM
23 October 2026, 10:39 am

“Uchumi wa mkoa wa Katavi unakua kwa kasi na kumekua na muingiliano mkubwa wa watu“
Na. Leah Kamala
Wananchi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kuimarisha juhudi za kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa zilizopo katika jamii ili kukabiliana na changamoto ya umaskini.
Wakizungumza na Mpanda radio fm, kuhusu siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini duniani, wananchi wameelezea sababu zinazochangia umaskini ikiwemo ukosefu wa ajira.
Nae Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi, Willison Kennedy amesema kuwa vikundi vya kijamii vina nafasi muhimu katika kukuza fursa za maendeleo kwa kuwawezesha wananchi kuanzisha shughuli za pamoja za uzalishaji.
Akizungumzia hali ya uchumi wa mkoa wa katavi kwa sasa, Dennis Bundale ambaye ni mchumi wa mkoa wa katavi amesema uchumi upo juu ukilinganisha na nyuma kwani fursa nyingi zilizopo ndani ya mkoa wa katavi zimeweza kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.
Kutokomeza umaskini kunahitaji ushirikiano wa serikali, jamii na wadau wa maendeleo pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika maendeleo.