Mpanda FM

Wanawake wa Katavi chukueni hatua zenye tija

19 November 2026, 10:43 am

Mwanzilishi wa jukwaa la wanawake KATAVI WORTH WOMEN Bi. Leah Gawaza akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Almas Smart Studio

“tumekua na matukio mbalimbali ambayo yaligusa jamii na wanawake kwa ujumla lakini hili litakua zaidi ya yote“

Na. Restuta Nyondo

Wanawake mkoani Katavi wametakiwa kujiboresha katika sekta mbalimbali kupitia kwa wanawake waliofanikiwa kwa kuchukua hatua zenye tija ili kujiimarisha kiuchumi,kifamilia na jamii.

Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa jukwaa la wanawake wa thamani Katavi Worth women Bi. Leah Gawaza wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa manspaa ya Mpanda kuhusu tukio la chukua hatua linalotarajiwa kufanyika tarehe 28 November mwaka huu.

Wanawake waliojitokeza katika kikao cha waandishi wa habari.

Leah ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tukio hilo muhimu ambalo pia litajikita katika kutoa tuzo kwa wanawake waliofanya vizuri katika sekta zao kwa mwaka 2026 na kutoa mitaji kwa wanawake 10 wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kujiinua kiuchumi.

Sauti ya Leah Gawaza

Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kikao hicho wamesema kuwa wamekua wakinufaika na jukwaa hilo kupitia elimu wanayopata,kutangaza biashara zao na kupata fursa mbalimbali.

Sauti ya wanawake

Hili ni tukio la 7  tangu kuanzishwa kwa jukwaa la Katavi Worth Women mwaka 2022 ambapo mpaka sasa lina zaidi ya wanawake  1500 kila mwaka limekua likibeba dhima mbali mbali na mwaka 2026 linaongozwa na dhima isemayo CHUKUA HATUA.

Baadhi ya wanawake wa thamani waliojitokeza katika kikao kilichofanyika 18 November