Mpanda FM

Wiki ya Mwanakatavi kutatua kero za wananchi

25 October 2026, 4:02 pm

Waziri wa Tamisemi akihutubia wananchi waliojitokeza katika maonesho ya wiki ya Mwanakatavi oktoba 25,2026. Picha na Mussa

“nimefurahi kuwaona wafanyabiashara kutokea Dodoma wameleta bidhaa zao hapa hii inaashiria maonesho haya yanakua na yanaweza kuwa ya kitaifa“

Na. Restuta Nyondo

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Tamisemi  profesa Riziki Shemdoe amewaagiza watendaji wa serikali kutatua kero za wananchi kupitia maonesho ya wiki ya mwanakatavi.

Akizungumza wakati akizindua maonesho hayo katika viwanja vya Mizengo pinda vilivyopo kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi ambapo amesema kuwa kila mwananchi apewe huduma bora na kutatuliwa changamoto zake kwa wakati.

Sauti ya waziri Shemdoe

Aidha Waziri Shemdoe ametangaaza viwanja hivyo kuwa eneo rasmi la maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi huku akipokea ombi la mkoa kuendelea shughulikia uwanja huo kuwa eneo la maonesho ya nane nane kanda ya magharibi.

Awali akizungumzia lengo la kuanzishwa kwa maonesho hayo mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametaja mafanikio ya kiuchumi na kijamii kwani wananchi wamekua wakiunganishwa katika sekta ya kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara kwa kupata fursa za uwekezaji, masoko na kujifunza teknolojia za kisasa.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi

Maonesho ya wiki ya mwanakatavi yameanza rasmi tarehe 25 October hadi tarehe 31 ambapo yanaongozwa na kauli mbiu isemayo Katavi yetu imarisha uchumi tekeleza dira ya taifa 2050.