Mpanda FM
Mpanda FM
6 October 2026, 1:13 pm

Mtoto Elias Luhenge, mwenye umri wa miaka 10, amefariki dunia katika Mtaa wa Rungwa, Kata ya Kazima mkoani Katavi, katika tukio linalodaiwa kuwa la kujinyonga.
Na Mwandishi wetu
Elias, mwanafunzi wa darasa la nne, amefariki wakati akitarajiwa kuanza mitihani ya darasa leo, huku tukio hilo likiwashtua ndugu, jamaa na majirani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu, huku taratibu za mazishi zikikamilika.