Mpanda FM
Mpanda FM
4 November 2026, 1:24 pm

“muhimu kufuatilia taarifa zote za hali ya hewa na kuzingatia kanuni bora za kilimo“
Na. Restuta Nyondo
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amezindua rasmi msimu wa kilimo wa mwaka 2026/2027 kwa kuwataka wakulima kutumia elimu, mbinu na teknolojia za kisasa walizojifunza katika wiki ya Mwanakatavi ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao.
Uzinduzi huo umefanyika katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mwanakatavi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mizengo Pinda, Kabungu, wilayani Tanganyika.
Akizungumza katika hafla hiyo Mrindoko amesema sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika uchumi wa mkoa wa Katavi ambapo inachangia asilimia 90 ya pato la mkoa na kutoa ajira kwa asilimia 85 ya wananchi.
Amesema katika msimu wa mavuno wa mwaka 2025/2026, Mkoa wa Katavi ulizalisha jumla ya tani milioni 1.5 za mazao, zikiwemo tani milioni 1.4 za mazao ya chakula, tani 108,931 za mazao ya biashara na tani 7,079 za mazao ya bustani.