Mpanda FM
Mpanda FM
24 November 2026, 11:20 am

“kuwa karibu na mtoto wako kwa kujenga urafiki naye ili kujua changamoto anazopitia“
Na. Leah Kamala
Wazazi na walezi mkoani Katavi wametakiwa kujenga ukaribu na watoto wao kipindi hiki cha likizo kwa kuwapatia muda wa kutosha na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo ili kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili.
Wito huo umetolewa na Sajenti Zainabu Omary kutoka dawati la jinsia na watoto kuwa wazazi wanapaswa kutumia muda huu wa likizo kuwafatilia watoto shughuli wanazofanya, na kujenga mawasiliano mazuri baina yao.
Sajenti Zainabu ameongeza kuwa suala la malezi sio la mzazi mmoja, hivyo baba na mama wanapaswa kushirikiana kwa pamoja kuwalea watoto katika maadili.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi na walezi wameeleza kuwa wamekuwa wakitenga muda wa kukaa na watoto kuzungumza nao na kufatilia mienendo yao ili kuhakikisha wanakuwa salama kipindi chote cha likizo.
Ni muhimu kwa wazazi na walezi kutumia kipindi hiki cha likizo kuimarisha mawasiliano na kuhakikisha watoto wanapata malezi na ulinzi unaostahili.