Mpanda FM

Leseni 7 za uchimbaji madini zafutwa Katavi

20 November 2026, 4:12 pm

Waziri wa Madini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibindi halmashauri ya Nsimbo .Picha na Leah Kamala

“tutakua walipa kodi wazuri kama ambavyo mnawapa sifa wawekezaji kuwa wanalipa vizuri“

Na Leah Kamala

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameelekeza kufutwa kwa leseni kubwa saba ikiwemo Leseni ya Uchimbaji wa Kati (ML) na Leseni za Utafiti (PL) mkoani KatavI ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Maelekezo hayo, yametolewa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde wakati akigawa leseni kwa vikundi tisa (9) vya wachimbaji wadogo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya (MBT) ikiwa ni mpango kufuta leseni ambazo hazifanyiwi kazi na kutolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye uhitaji maalumu.

Sauti ya waziri Mavunde

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph Kimaro ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuwapatia leseni vijana na kuahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya wizara.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpanda

Kwa upande wake afisa madini mkoa wa katavi Ernest Sanka amesema tayari vikundi vinne ambavyo mchakato wa kupatiwa leseni unaendelea  ikiwemo  maneneo hayo yanaghawiwaa kwa haki na usawa

Sauti ya afisa madini

Nao baadhi ya wachimbaji wamepongeza hatua aliyoifanya waziri wa madini kwani itasaidia kupata maeneo ya uchimbaji na kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya wachimbaji
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jmaila Yusph Kimaro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibindi