Mpanda FM
Mpanda FM
20 November 2026, 4:25 pm

“Siku ya wanaume duniani ni siku inalenga katika kutambua mchango wa mwanaume katika familia,jamii na taifa “
Na. Leah Kamala
Wananchi mkoani katavi wametoa maoni yao kuhusiana na siku ya wanaume duniani kwa kutambua nafasi ya wanaume katika maendeleo ya familia na ujenzi wa jamii yenye maadili.
Wakizungumza na mpanda radio fm, kwa nyakati tofauti wananchi hao wameeleza kuwa mwanaume ni kama mshauri, na husimama katika nyanja zote ili kuhakikisha familia inakidhi mahitaji yake.
Akizungumzia umuhimu wa siku hiyo, Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda Malagano Thabit amesema mwanaume ana mchango mkubwa katika malezi ya familia, kujenga jamii bora pamoja na kutoa mwongozo kwenye shughuli za maendeleo ya kijamii.
Aidha Thabit ametoa wito kwa wanaume kuwa mfano bora katika majukumu ya kifamilia, na kuwaheshimu wanawake ili kujenga jamii yenye upendo amani na mshikamano.