Mpanda FM
Mpanda FM
1 October 2026, 3:46 pm

“Walimu wakipata motisha mbalimbali ufaulu utaongezeka“
Na. Restuta Nyondo
Shirika lisilo la kiserikali Green Leaf Organisation limetoa mashine za kutolea kopi 4 zenye thamani ya shilingi 7,200,000 na kiasi cha shilingi 3,000,000 kwaajili ya uwezeshaji wa miradi ya ufugaji na kilimo katika shule za sekondari halmashauri ya Tanganyika ili kuongeza tija ya ufundishaji,ujifunzaji na lishe bora.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya fedha ya shilingi milioni tatu katika shule za sekondari Mpandandogo, Sibwesa na Ilandamirumba na mashine za kutolea kopi kwa shule Kasekese, Ikola, Majalila na Kamsanga mratibu wa mradi wa Teachers Shujaa, Inua Mwalimu, Inua elimu Bw. Donath Kasirika amesema kuwa lengo ni kuendelea kurahisisha utendaji kazi wa walimu katika shule zao na kuleta tija kitaaluma.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika Reginald Valence ameipongeza shirika hilo na kumuagiza afisa elimu kufutilia kwa karibu matumizi ya fedha zilizotolewa na kuleta matokeo Chanya katika shule hizo.
Aidha walimu wakuu wa shule zilipokea msaada huo wamesema kuwa itaongeza motisha na ufanisi katika utendaji kazi wao huku wakiahidi kufanya matumizi sahihi na kuongeza mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Mradi wa Teachers Shujaa ,Inua Mwalimu, Inua elimu unatekelezwa katika shule 23 za sekondari katika halmashauri ya Mpimbwe na Tanganyika mkoani Kataviambapo mradi huo umefadhiliwa na Mtandao wa elimu Tanzania (TENMET).