Mpanda FM
Mpanda FM
19 October 2026, 11:05 am

“kwasasa tumefanikiwa kuzifikia zaidi kaya masikini zinazohudumiwa na Tasaf lakini bima hii ni ya kila mtu“
Na. Samwel Mbugi
Wananchi mkoa wa wa katavi wametakiwa kujiunga na bima ya afya kwa wote itakayoenda kusaidia watanzania wote wenye vipato vya chini ili kupata matibabu bila changamoto yoyote.
Akizungumza na Mpanda radio fm afisa mwananchama mwandamizi Mohamed Katoto amesema bima imewalenga wananchi wote ili waweze kunufaika na matibabu ambayo yangeweza kugharimu fedha nyingi.
Katoto amesema bima ya afya kwa wote itazinduliwa rasmi ili kuanza kusajili kaya ambazo zitakuwa na sifa ya kupata bima hiyo ambayo wataweza kupata matibabu nchi zima ndani ya Tanzania
Ikumbukwe kuwa Bima ya afya ni mfumo unaowezesha kupata huduma za matibabu bila kulipa fedha taslimu kila unapohitaji matibabu nchini.