Mpanda FM
Mpanda FM
30 October 2026, 11:41 am

“mkoa wa Katavi bado kuna madereva ambao wanasababisha ajali kwa makosa ya kibinadamu“
Na. Leah Kamala
Wananchi mkoani Katavi wameiomba jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kuendelea kutoa elimu ili kupunguza ajali zinazotokea na kulinda maisha ya raia.
Wakizungumza na mpanda radio fm, wananchi hao wamesema kuwa kutozingatia sheria kunaweza kuchangia kuongezeka kwa ajali za barabarani.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Katavi kamishna msaidizi wa jeshi la polisi ACP Leopord Fungu amezungumzia mikakati iliyowekwa na inavyoweza kusaidia kupunguza ajali.
Aidha Fungu ametoa wito kwa watumiaji wa barabara mkoa wa Katavi kuheshimu na kufuata kanuni za usalama barabarani