Mpanda FM

Kutotekelezwa kwa sheria ya misitu kunavyochochea ukataji holela wa misitu Katavi (sehemu ya tatu)

11 September 2026, 10:49 am

mto uliopokatika kijiji cha singililwa kuelekea eneo la mgodi. Picha na Restuta

sio tu uharibifu wa misitu Katavi kuna uharibu mkubwa wa vyanzo vya maji

Na Restuta Nyondo

Karibu kusikiliza sehemu ya tatu ya makala inayoangazia utekelezaji kifungu cha sheria ya misitu 20002 na kifungu cha 81 cha sheria ya usimamizi wa mazingira 2004 kunasababisha ukataji holela wa misitu na kuharibika kwa mapitio ya wanyamapori kutokana na upanuzi wa eneo la uwekezaji KMCL hali iliyosababisha migogoro kati ya binadamu na wanyamapori na uharibifu wa vyanzo vya maji mkoani Katavi.

Katika sehemu hii ya tatu ya Makala haya inaangazia suluhisho juu ya uharibifu na ufyekaji wa misitu na kukabiliana na athari zinazojitokeza.

Elimu kwa wawekezaji  na usimamizi wenye mkazo wa sheria unatajwa kuwa Suluhu la tatizo la uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za uchimbaji wa madini.