Mpanda FM

Makonda: Watendaji wazembe serikalini wanakiangusha chama

5 February 2024, 3:49 pm

Chama cha mapinduzi hakipo tayari kuona Wananchi wakiendelea kuteseka na kero zinzowakabili huku watendaji wa serikali wakitumia mianya hiyo kujinufaisha wenyewe bila kujali wananchi.Picha na Deus Daud

Na Festo Kinyogoto

Mjumbe wa halamashauri kuu ya CCM taifa, katibu itikadi uenezi na mafunzo Chama cha Mapinduzi ndugu PAUL MAKONDA amewaasa watendaji waserikali kuwapa Wananchi kipaumbele katika utoaji huduma na kuacha tabia ya kutanguliza maslahi yako binafsi.

Makonda ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyaka katika viwanja Vya Kashaulili Manispaa ya Mpanda mkoa Katavi kuwa, chama cha mapinduzi hakipo tayari kuona Wananchi wakiendelea kuteseka na kero zinzowakabili huku watendaji wa serikali wakitumia mianya hiyo kujinufaisha wenyewe bila kujali wananchi.

Sauti ya Mjumbe wa halamashauri kuu ya CCM taifa, katibu itikadi uenezi na mafunzo Chama cha Mapinduzi ndugu PAUL MAKONDA

Makonda amsema watendaji wote wa Serikali wanapaswa kushugulika na matatizo ya Wananchi na kuacha tabia ya kusubili kipindi ha uchaguzi kuwalaghai wananchi kwa kutoa Kanga na Rushwa kwani utawala bora ndio unawapa imani wananchi haki na ustwai wa taifa.

Sauti ya Mjumbe wa halamashauri kuu ya CCM taifa, katibu itikadi uenezi na mafunzo Chama cha Mapinduzi ndugu PAUL MAKONDA

Makonda amewasili leo mkoa Katavi akitoka mkoa wa Kigoma katika ziara iliopewa jina la mikoa 20 back to back kwajili ya kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kutafuta suruhu ambapo ataelekea mkoani Rukwa.