Mpanda FM

Mafunzo ya ujasiriamali yahitimishwa Katavi

18 August 2023, 10:18 am

Kufuatia mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na Mpanda Radio fm kwa kushirikiana na Mkwawa Vocation Training Center washiriki wa mafunzo hayo wamekiri mafunzo hayo yatawainua kiuchumi.

Wameyasema hayo mara baada ya kutamatika kwa mafunzo hayo Agosti 17, 2023 na kubainisha namna ambavyo mafunzo hayo yatakavyowasaidia.

Awali akitoa mafunzo hayo Mkufunzi wa mafunzo hayo Benjamini Chahe amesema mafunzo hayo aliyoyatoa wakiyazingatia yatasaidia kuongeza kipato cha wajasiriamali hao kwani ni watu wengi wamefanikiwa kupitia mafunzo kama hayo aliyoyatoa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mpanda radio fm Eliakim Sadoki ametoa pongezi kwa wakufunzi pamoja na washiriki wa mafunzo hayo na kueleza kuwa yatasaidia kuongeza kipato cha familia.

Akifunga mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Respista Kalugendo akimuwakilisha Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda ,amewataka Wajasiriamali hao kuunda vikundi vya pamoja na kujisajili ili waweze kutambulika kisheria na kuwa na sifa za kukopesheka.

Mafunzo hayo ya ujasiriamali yameanza kutolewa august 15 na kutamatika august 17 2023 Lengo likiwa ni kutoa ujuzi kwa jamii ili waweze kuongeza wigo mpana wa kujipatia kipato na kuhimarika kiuchumi.

#mpandaradiofm97.0