Mpanda FM

Huduma Mkoba Kuimarisha Zoezi la Chanjo ya Uviko 19

20 November 2021, 11:35 am

Serikali mkoani katavi imekuja na mpango  harakishi na shirikishi wa kutoa  huduma mkoba  ya uviko19 ambavyo itawasaidia wananchi kupata chanjo hiyo  popote  pale walipo.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkao wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko   ambapo ameeleza kuwa wamekuja na huduma hiyo katika kuhakikisha   wananchi walio mbali na vituo vya afya  wananpata chanjo hiyo.

Aidha Mrindoko amesema kuwa vituo vya kutolea huduma ya chanjo ya uviko 19  vimeongezeka kutoka vituo 45  hadi 86.

Hata hivyo mrindoko ameomba wananchi kupuuza maneno yote  yanatolewa na watu yakilenga kupotosha jamii  kuhusu chanjo ya uviko 19  huku akitanabaisha kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na wataalam wa afya.