Mpanda FM

Shule ya Msingi Msasani kunufaika na milioni 14 ya matundu ya vyoo

15 December 2023, 2:40 pm

Mfano wa tundu la choo. picha na Mtandao

Serikali yachangia shilingi milioni 14 kwa ajili ya matundu ya vyoo shule ya Msingi Msasani.

Na Gladness Richard – Mpanda

Kufuatia ujenzi unaoendelea  Wa shule ya Msingi Msasani Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Serikali imechangia shilingi milioni 14 kwa ajili ya matundu ya vyoo.

Akizungumza na Mpanda Radio FM mwenyekiti wa mtaa wa Msasani amesema wakati ujenzi  wa darasa ukiendelea wamepokea kiasi cha fedha Ili madarasa yanavokamilika na matundu ya vyoo yaweze kukamilika.

Kwa upande wao wananchi wa mtaa wa msasani wamesema kuwa kukamilika kwa  ujenzi wa shule hiyo  kutafungua fursa  kwa jamii inayozunguka eneo hilo.

Sauti ya Wananchi

Shule ya Msingi Msasani inajengwa kwa nguvu za wananchi ambapo inavyumba viwili vya madarasa na ofisi moja huku inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwaka 2024.