Mpanda FM

TAKUKURU Katavi yawafikisha 7 mahakamani kwa wizi wa bilioni 1.2

25 August 2023, 10:25 am

KATAVI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Katavi imewafikisha mahakamani watumishi wa serikali 7 kwa makosa matatu ikiwemo wizi wa fedha zaidi ya bilioni 1.2.

Kelvin Mwaja ni mwanasheria kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoa wa Katavi amesema kuwa watuhumiwa walitenda makosa hayo mwaka 2022 na 2023 .

Wakisomewa mashtaka yao Mara baada ya kufikishwa mahakamani mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Katavi Gway Sumayi ambapo watuhumiwa hao ni Canuthe Hipolite Matsindiko (muhasibu) ,Michael Mathew Katanga (muhasibu), Masami Andrew Mashauri (muhasibu), tumaini Richard Misese , Maira Samson Oluomba muhasibu,Emmanuel Damas Salanga (muhasibu) na Laurent William Sunga.

Watuhumiwa wote wanakabiliwa na mashtaka ya kuunda genge la kiarifu,wizi wa fedha Zaidi ya bilioni 1.2 na utakatishaji wa fedha za serikali katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Katavi Gway Sumayi amesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa dhamana au kusikiliza kesi hiyo hivyo imepelekwa katika mahakama kuu ya kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Kesi hiyo imesikilizwa tarehe 21 mwezi huu ambapo inatarajiwa kusikilizwa tena tarehe 04 mwezi 9 mwaka huu katika mahakama kuu ya kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

#mpandaradiofm97.0

#TAKUKURU