Mpanda FM

Katavi: Kusafirisha asali lazima kibali

30 June 2023, 10:24 am

KATAVI

Wafanyabiashara wa mazao ya nyuki manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wemetakiwa kufuata taratibu na sheria za usafirishaji wa mazao ya nyuki ikiwamo kuwa na vibali vya usafirishaji.

Mpanda Radio Fm imezungumza na wafanyabiashara wanaojihusisha na uuzaji wa asali ili kutambua njia wanazozitumia katika kuifanya biashara hiyo na kueleza kuwa kufuata miongozo ya kuwa na vibali na kuzingatia usafi wa mali inayosafirishwa kunasaidia kuepusha migogoro na mamlaka zinazotoa vibali vya usafirishaji.

Afisa Nyuki Msaidizi kutoka Wakala wa Huduma ya Misitu TFS wilaya ya Mpanda William Lukas Molllel amesema kuwa sheria, kanuni na taratibu za usafirishaji wa mazao ya nyuki zikifuatwa zitasaidia kuepusha migongano baina ya mamlaka na wafanyabiashara.

#mpandaradiofm97.0

#tfs