Mpanda FM

Dirifu walia ukosefu huduma ya maji

7 June 2023, 10:28 am

MPANDA

Wananchi wa kijiji cha Dirifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamezitaka mamlaka za maji kupitia serikali ya mkoa kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa kipindi kirefu.

Hayo yamewasilishwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho wakati akizungumza katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ambapo amesema changamoto ya maji imekuwa kikwazo katika shughuli mseto za wananchi kijijini hapo.

RC Mrindoko amemtaka mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kutatua changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa kijiji hicho.

#mpandaradiofm97.0

#ruwasa

#wizarayamaji