Mpanda FM

Wakulima Kasokola walizwa na mifugo

24 August 2023, 8:39 am

MPANDA

Baadhi ya wakulima katika kata ya Kasokola halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia wafugaji kulisha mifugo kwenye mazao yao hali ambayo inawarudisha nyuma kiuchumi.

Wamebainisha hayo katika mkutano wa hadhara mbele ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kuwa wamekuwa wakitoa taarifa ngazi ya uongozi wa kijiji lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa mpaka sasa.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kasokola Christ Mwanawima amekiri kuwepo kwa mgogoro huo kwa muda sasa licha ya juhudi kadhaa zilizofanywa na serikali ya kata.

Kufuatia Hali hiyo mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ameliagiza jeshi la polisi wilaya ya Mpanda kuwakamata waliolalamikiwa na kuwapeleka katika vyombo vya sheria.

Kwa mara kadhaa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini imekuwa ikilipotiwa licha ya serikali kuendelea kuchukua hatua ya kutatua migogoro hiyo.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayamifugonauvuvi