Mpanda FM
Mpanda FM
9 September 2025, 8:57 pm

Baadhi ya wanachama waliojitokeza kwenye mkutano wa mgombea mwenza wa urais. Picha na Samwel Mbugi
“Chama kikipewa ridhaa kitaendelea kuboresha huduma za kijamii”
Na Samwel Mbugi
Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi amesema chama kikipewa ridhaa ya kuongoza nchi kitaendelea kuboresha sekta zote muhimu ikiwemo sekta ya afya.
Balozi Nchimbi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Majimoto mkoa wa katavi ambapo amesema dhamira ya mgombea wa nafasi ya Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuwaletea maendeleo kwa kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na makazi yao kwa kujenga na kuboresha vituo vya afya, shule na barabara.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Idd Kimanta amesema ushindi wa chama kwa mkoa wa Katavi ni lazima.
Ikumbukwe kuwa uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais utafanyika October 29 mwaka huu.