Mpanda FM

Vijana Mkoani Katavi wametakiwa kufanya kazi ili wajikwamue kiuchumi

3 April 2024, 1:02 pm

picha na Mtandao

Ni muhimu vijana kushiriki katika kufanya kazi ili kusaidia kuondoa makundi ya kiharifu

Na Veronika Mabwile -Katavi

Imeelezwa kuwa uwepo wa baadhi ya vijana wasioshiriki katika shughuli za Kiuchumi katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatokana kutokuelezwa madhara yatokanayo na kutokufanya kazi

Hayo yameelezwa na baadhi ya Wakazi wa Manispaa  ya Mpanda wakati  wakizungumza na Mpanda Redio Fm na kusema kuwa chanzo cha uwepo wa baadhi ya Vijana wasiowajibika katika shughuli za Kiuchumi  inachangiwa na malezi katika familia.

Sauti za Wananchi manispaa ya Mpanda wakizungumza

Afisa Ustawi wa Jamii Anyurumie Longo amesema ni muhimu vijana kushiriki katika kufanya kazi ili kusaidia kuondoa makundi ya kiharifu

Sauti ya Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Mpanda

Uwepo wa Vijana wasioshiriki katika  shughuli za kiuchumi unachangia kuwepo kwa makundi ya kiharifu katika jamii hivyo vijana wamehimizwa kufanya kazi za kujipatia kipato .