Mpanda FM

Katavi, Wafanyabiashara 24 Mbaroni Kupandisha bei ya Sukari

19 March 2024, 3:19 pm

Picha na Mtandao

Ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuzingatia bei  elekezi inayotolewa na Serikali ili kupunguza usumbufu kwa mlaji

Na Betord Benjamin-Katavi

Jumla ya Wafanyabiashara 24 Katika Manispaa ya Mpanda Mkoani  Katavi wamekamatwa kutokana na kuuza sukari kinyume na bei elekezi iliyotolewa na Serikali. 

Akijibu swali la baadhi ya Wafanyabiashara  waliohoji juu ya hali ya mwenendo wa bei elekezi ya Sukari Afisa biashara Manispaa ya  Mpanda  Paul Kahoya  amesema ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuzingatia bei  elekezi inayotolewa na Serikali ili kupunguza usumbufu kwa mlaji

Sauti ya Afisa biashara Manispaa ya  Mpanda  Paul Kahoya.

Akizungumza kwa Niaba ya  Mkuu wa mkoa   wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko  Mkuu wa Wilaya ya  Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wafanyabiashara  Mkoani hapa kufanya shughuli hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni  zilizowekwa na serikali  ikiwa ni pamoja na kulipa kodi.

Sauti ya Onesmo Buswelu kaimu mkuu wa mkoa wa Katavi.

Kulingana na bei elekezi ya serikali kilo ya Sukari Mkoani hapa inatakiwa kuuzwa kwa Tshs 3,200 ambapo mfuko wa sukari wa kilo 50 unatakiwa kuuzwa kwa Tshs 145,000