Mpanda FM

23 May 2022, 2:27 pm

MPANDA

Vijana Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kujishughulisha na kilimo kwa kujiunga na vikundi ili kulima kilimo chenye tija zaidi.

Hayo yamesemwa na wakulima wa kikundi cha AMAKWAWO wanaojishughulisha na kilimo cha zao la nyanya Wilayani Mpanda na kusema kuwa  vijana wapaswa kujiunga na vikundi vya kilimo kwa lengo la kujikimu kimaisha na kupata fursa ya mikopo ya asilimia 10 kutoka serikalini.

Benatus Ngoda ambaye ni Afisa kilimo Manispaa ya Mpanda amesema ili vijana kunufaika na kilimo wanapaswa kujiunga na vikundi na kurahisisha kupata soko la pamoja sambamba na kufikiwa na wataalamu wa kilimo kwa urahisi zaidi.

Kikundi cha AMAKWAWO chenye maana ya Amani na Maendeleo Kwa watu wote kilianzishwa mwaka 2014  kikijikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda.