Mpanda FM

Mkoa wa Katavi umefanikiwa kupokea zaidi ya Bilioni 800 katika utekelezaji wa Miradi Mbalimbali.

27 November 2023, 12:05 pm

Kamati ya Siasa ikiwa katika kijiji cha Kakese wakikagua Mradi wa Maji .Picha na Betord Benjamini

Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi (CCM ) kwa mwaka 2020 hadi 2025 katika kipindi cha Miaka Miwili kuanzia 2022 hadi September 2023.

Na Ben Gadau -Katavi

Kamati ya Siasa Mkoa wa Katavi ikiongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya Kikao kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama kwa mwaka 2020 hadi 2025 katika kipindi cha Miaka Miwili kuanzia 2022 hadi September 2023.

Akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama ,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema katika kipindi cha Miaka Miwili Mkoa wa Katavi umefanikiwa kupokea zaidi ya Bilioni 800 katika utekelezaji wa Miradi Mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko .Picha na Betord Benjamini

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko

Idd Kimanta ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Katavi amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa usimamizi katika utekelezaji wa ilani hiyo huku akiendelea kuwataka Watumishi Mbalimbali kuwa wa moja katika utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ili kuwaletea Maendeleo Wananchi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Iddi Kimanta .Picha na Betord Benjamini

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Katavi