Mpanda FM

Buswelu: waumini endeleeni kupinga matendo maovu kwenye jamii

26 September 2023, 5:47 pm

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akizungumza na waumini wa madhehebu, Picha na Anna Milanzi

Na Veronica Mabwile – Katavi
Waumini wa madhehebu mbalimbali Mkoani Katavi wameombwa kuendelea kupinga matendo maovu yanaojitokeza katika jamii ikiwemo kamchape na lambalamba ili kuendelea kulinda amani iliyopo .

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko katika kanisa la Victorius Church wakati wa harambee ya ununuzi wa kiwanja cha kanisa.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu

Kwa upande wake mchungaji wa kanisa hilo Shubi Yosia akizungumza mara baada ya Harambee hiyo amewashukuru washiriki katika zoezi hilo na kuutaja mchango wa madhehebu ya dini katika jamii kuwa ni Pamoja na kuhakikisha jamii inabadilika kutoka katika mambo yasiyofaa .

Sauti ya Mchungaji wa Kanisa Shubi Yosia

Pamoja na hayo Buswelu ameiomba jamii kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita ikiwa ni pamoaja na ujenzi wa miradi ya maendeleo