Mpanda FM

Waliochomewa tumbaku Mpanda kutafutiwa ufumbuzi

28 March 2024, 1:18 pm

Katika uvamizi huo jumla ya majengo kumi ya kukaushia Tumbaku yamechomwa moto pamoja na stoo mbili pamoja na wananchi hao kuchukuliwa mali zao ikiwemo simu za mkononi pamoja na fedha.Picha na Betord chove

Na Bertod Chove-katavi

Serikali wilayani Mpanda imewahakikishia wananchi wa kijiji cha Mtambo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kulitafutia ufumbuzi changamoto waliokutana nayo ya kuvamiwa eneo wanalofanyia shughuli za kilimo na kuamrisha kuchoma tumbaku na kuwapiga.

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph Akizungumza Alipofika na kutathimini madhara yaliyotokana na tukio hilo amewataka wananchi hao kuacha kufanya shughuli katika maeneo ya hifadhi ili wawe salama na kulinda hifadhi zilizotengwa kwenye msitu wa north east Mpanda.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph Akizungumza Alipofika na kutathimini madhara yaliyotokana na tukio hilo”

Awali  wakizungumza na Mpanda radio fm baadhi ya waaathirika wanaofanya shughuli katika eneo hilo wameeleza namna tukio lilivotokea na kuiomba serikali kuwasaidia kutokana na hasara waliyoipata ikiwa zao hilo lilikuwa chanzo pekee cha mapato .

 

Sauti ya baadhi ya waaathirika wanaofanya shughuli katika eneo hilo wameeleza namna tukio lilivotokea na kuiomba serikali kuwasaidia kutokana na hasara waliyoipata

Baadhi ya mashamba yaliyochomwa moto na kusababisha hasara kwa wakulima hao”. Picha na Betord Chove

Katika hatua nyingine Damas Ngasa afisa ardhi halmashauri ya Nsimbo na  Baraka Abdalah Afisa mhifadhi Misitu Katavi wakizungumza wamethibitisha kuwa eneo hilo ni la hifadhi ambalo haliruhusu kufanyika kwa shughuli za kibinadamu na kusema kuwa hakuna operesheni yeyoteiliyofanyika hivi karibuni katika eneo hilo.

Sauti ya Damas Ngasa Afisa ardhi halmashauri ya Nsimbo na  Baraka Abdalah Afisa mhifadhi Misitu Katavi wakizungumza wamethibitisha kuwa eneo hilo ni la hifadhi

Katika uvamizi huo jumla ya majengo kumi ya kukaushia Tumbaku yamechomwa moto pamoja na stoo mbili pamoja na wananchi hao kuchukuliwa mali zao ikiwemo simu za mkononi pamoja na fedha.