Mpanda FM

Jamii yaaswa kutofumbia macho vitendo vya ukatili

10 June 2023, 3:32 pm

MPANDA

Kukosa elimu ya ukatili wa kimwili kumetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea watu wa karibu kushindwa kuripoti matukio ya ukatili wa kimwili kipindi yanapotokea.

Hayo yamebainishwa na wakazi wa manispaa ya Mpanda wakati wakizungumza na kituo hiki na kuongeza kuwa elimu zaidi inapaswa kutolewa na watu kuacha kufumbia macho vitendo hivyo.

Kwa upande wake Fujensia Kapama wa Mkombozi Parallegal amesema kuwa watu waache desturi kandamizi na kuwa wazi kuzungumza matukio haya ya ukatili yanapotokea.

Judith Mbukwa Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoani Katavi amesema kuwa wameweka mazingira rafiki kwa watu wanaokwenda kutoa taarifa kituoni hapo hivyo kuwasihi watu kuacha uoga na kuwaasa wanaume kujitokeza katika kuripoti matukio hayo.

Kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu Tanzania ya mwaka 2022 (LHRC) watu wa karibu wanaaminika kwa asilimia 60 kwenye utatuzi wa migogoro (ukatili) lakini sio kwa makosa ya jinai.

#mpandaradiofm97.0

#katavists

#dawatilajinsianawatoto