Mpanda FM

Wakulima waaswa kuchukua mbolea mapema

11 September 2023, 8:27 am

MPANDA
Wakulima halmashauri ya Mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kuchukua mbolea mapema ili kuepukana na changamoto ambazo zilitokea katika msimu wa kilimo uliopita.

Afisa kilimo Manispaa ya Mpanda Gwalusajo Kapande amesema kuwa zoezi la ununuzi wa mbolea limeanza Septemba 1, 2023 hivyo wakulima wameshauriwa kununua mbolea ili kuepuka matumizi holela ya mbolea.

Kwa upande mwingine amesema wamejipanga kufikisha mbolea katika maeneo husika ya kilimo, ili kuepusha changamoto ya wakulima kufuata mbolea katika maeneo ya mjini ambapo walikuwa wanatumia gharama kubwa.

Wakulima wamewaomba maafisa kilimo kutoa elimu zaidi juu ya matumizi ya mbolea wakihusisha na hasara ambazo baadhi wamepata katika msimu wa kilimo uliopita kutokana na matumizi mabaya ya mbolea.
#mpandaradiofm97.0
#wizarayakilimo