Mpanda FM

RC Katavi awasihi bodaboda kutunza amani

6 June 2025, 3:27 pm

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akitoa neno kwa bodaboda. Picha na Samwel Mbugi

“Nyie ni nguzo kubwa ya usalama katika mkoa wetu”

Na Samwel Mbugi

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka bodaboda mkoa wa Katavi kutokutumika kuvuruga amani na usalama.

Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa umoja wa bodaboda mkoa wa Katavi uliofanyika ukumbi wa polisi uliopo manispaa ya Mpanda wenye ajenda mbalimbali ikiwemo Katiba ya umoja huo.

Sauti ya mkuu wa mkoa

Mrindoko amewataka bodaboda kushirikiana na viongozi wa serikali na vyombo vya usalama katika kulinda amani na utulivu kwa kufichua maovu kabla hayajaleta madhara makubwa kwa wananchi.

Sauti ya mkuu wa mkoa

Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodaboda mkoa wa Katavi Isack Daniel Joseph amesema kuwa watakuwa bega kwa bega na viongozi wa serikali katika kuhakikisha utulivu na usalama unakuwepo ndani ya mkoa wa Katavi hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Sauti ya mwenyekiti wa bodaboda

Umoja wa bodaboda umefanya mkutano mkuu ambao ulijumuisha viongozi wa kanda zote za mkoa na viongozi wa maegesho yote pamoja na viongozi wa serikali.