Mpanda FM
Mpanda FM
6 June 2025, 3:46 pm

Mganga mkuu wa manispaa ya Mpanda Dr. Paul Swakala. Picha na Edda Enock
“Hatufahamu huu ugonjwa unasababishwa na nini”
Na Edda Enock
Baadhi ya wanaume wa manispaa ya Mpanda mkoni Katavi wameiomba serikali kupitia wizara ya afya kuongeza juhudi za utoaji wa elimu kuhusu ugonjwa wa saratani ya tezi dume.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa hawana uelewa juu ya ugonjwa huo, dalili za awali za ugonjwa huo wala umuhimu wa kuchunguza mapema afya zao.
Akitaja sababu za ugonjwa wa saratani ya tezi dume Paul Swakala mganga mkuu manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amesema ni kutokufanya mazoezi, lishe hatarishi na umri mkubwa kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Aidha Swakala amewataka wanaume kufika katika vituo vya afya ili kuangalia afya zao na kuchukua hatua za mwanzo za kidaktari kwani idadi ya wagonjwa inaongezeka kwa kasi duniani kuanzia mwaka 2019 hadi sasa.
Saratani ya tezi dume hutokea pale chembe chembe hai za tezi kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili chembechembe hizi hutengeneza vimbe ndani ya tezi dume na hatimaye husambaa mwilini.