Mpanda FM

Sungusungu Mpanda wageuka vibaka

9 February 2024, 2:41 pm

Baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijitambulisha kuwa ni ulinzi shirikishi ambao wamekuwa wakinyang’anya mali za wananchi ambao wamekuwa wakikutana nao majira ya usiku. Picha na Mtandao.

Na John Benjamin-Katavi

Baadhi ya wananchi katika mtaa wa Airtel kata ya Uwanja wa Ndege halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani  Katavi wamelalamikia kuwepo kwa kundi ambalo limekuwa likijitambulisha kuwa ni ulinzi shirikishi ambalo limekuwa likifanya matukio ya kiharifu kama unyanganyi.

Wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa licha ya hali ya kiusalama kuwa shwari kumeibuka kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijitambulisha kuwa ni ulinzi shirikishi ambao wamekuwa wakiwanyanganya wananchi mali zao ambao wamekuwa wakikutana nao majira ya usiku

Sauti ya wananchi mtaa wa airtel wakilalamikia Sungusungu.

Mwenyekiti wa mtaa wa Airtel kata ya Uwanja wa  Ndege halmashauri ya manispaa ya Mpanda Jastin Lukensa amesema kuwa taarifa hizo hazijamfikia kuwepo kwa matukio hayo, na amekiri kuwepo kwa kusuasua kwa zoezi hilo la ulinzi shirikishi katika kata hiyo huku akitaja wananchi kushindwa kutoa mchango kwa ajili ya ulinzi shirikishi.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Airtel kata ya Uwanja wa  ndege halmashauri ya manispaa ya Mpanda Jastin Lukensa.

Jeshi la polisi mkoani Katavi limendelea kuhimiza kuundwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kuendelea kupambana na matukio ya kiarifu.