Mpanda FM

Kamati ya Siasa Mkoa wa Katavi  wameitaka Serikali kutoa elimu kwa Wafanyabiashara

27 November 2023, 12:59 pm

Viongozi wa Kamati ya Siasa Mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa katavi wa pili kushoto na Mkuu wa wilaya ya Mpanda wa pili kulia Na mwakilishi wa mwenyekiti Ccm mkoa ambaye ni katibu mwenezi Ccm mkoa Joseph lwamba wakitembelea Miradi katika wilaya ya Mpanda .Picha na Betord Benjamini

Serikali imetumia pesa kuwekeza ili Wafanyabiashara waweze kuwa na uelewa kuhusu ufanyaji kazi wa jengo hilo.

Na Betord Benjamini-Katavi

Kamati ya Siasa Mkoa wa Katavi  wameitaka Serikali kutoa elimu kwa Wafanyabiashara Mkoani Katavi kuhusu Umuhimu wa Kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi [CCM] Mkoa wa Katavi ambaye ni Katibu Mwenezi Chama Cha Mapinduzi Mkoa Joseph Lwamba amesema Serikali imetumia Pesa Kuwekeza ili Wafanyabiashara Waweze kuwa na Uelewa kuhusu Ufanyaji Kazi wa Jengo hilo

Sauti ya Katibu Mwenezi Chama Cha Mapinduzi Mkoa Joseph Lwamba akimuwakilisha Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Katavi

Awali Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila yusuph Wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga Fedha kwa ajili ya Jengo hilo na kuwataka  Wafanyabiashara kulitumia Jengo hilo ili liweze kuwanufaisha.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila yusuph

Kwa Upande wake Afisa biashara Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ameainisha dhima ya kuanzisha vituo Jumuishi Nchini na kusema kuwa Jengo hilo lilojengwa Manispaa ya Mpanda limegharimu kiasi cha Tshs Million 94.5.

 

Sauti ya Afisa biashara Manispaa ya Mpanda