Mpanda FM

Wananchi Katavi hawana elimu ya utunzaji wa kinywa, meno

21 March 2024, 10:55 am

Picha na Mtandao

Utafiti uliofanyika umegundua kuwa watoto  wenye umri wa miaka sita hadi tisa ndio waathirika wakubwa

Na Samwel Mbugi -Katavi

Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni  mseto kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno ambapo wameonesha kutokuwa na  elimu ya kutosha ya namna ya utunzaji wa kinywa na meno.

Hayo yamebainishwa na wananchi wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm ambapo wamesema kuwa hawana elimu ya afya ya kinywa na meno ambapo wameitaka mamlaka husika kuendelea kutoa elimu kila wakati bila kusubiri siku ya maadhimisho.

Sauti za Wananchi wakieleza kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya afya ya kinywa na meno

Kwa upande wake daktari  anayehusika na afya ya kinywa na meno Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi Rhoda Mwakasege amesema kuwa utafiti uliofanyika wamegundua kuwa watoto  wenye umri wa miaka sita hadi tisa ndio waathirika zaidi kwa kiasi kikubwa.

Sauti ya Daktari  anayehusika na afya ya kinywa na meno Manispaa ya Mpanda anaeleza watoto wengi ni waathiriwa wakubwa wa magonjwa ya meno

Pia amewataka wananchi kutokimbilia kutoa meno bila kufanya matibabu kwani kutoa meno inatakiwa kuwa  hatua ya mwisho baada ya matibabu kushindikana.

Sauti ya Daktari  anayehusika na afya ya kinywa na meno Manispaa ya Mpanda akieleza hatua za kuchukua unaposumbuliwa na meno

Ikumbukwe kuwa kilele cha maadhimisho ya afya ya kinywa na meno kimefanyika tarehe 20 mwezi wa tatu mwaka huu, kwa kaulimbiu inayosema kinywa chenye furaha ni mwili wenye furaha.