Mpanda FM

Wananchi Katavi watakiwa kushiriki uchaguzi

11 April 2024, 10:00 am

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Nassoro Kakulukulu akizungumza katika Swala ya Eid -Al- Fitr. Picha na Deus Daudi

Uchaguzi unapofika ni vema kushiriki katika uchaguzi huo na kuendeleza utulivu na amani iliyopoSheikh Nassoro Kakulukulu.

Na Deus Daudi-Katavi

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi Nassoro Kakulukulu amewataka Wananchi kujiandaa na kushiriki katika Uchaguzi Wa serikali za Mitaa  na Uchaguzi Mkuu  Mwaka ujao

Ameyasema hayo wakati wa Swala ya Eid- Al -Fitr kwa Waumini waliojitokeza katika Msikiti Mkuu wa Mkoa wa Katavi amesema Uchaguzi unapofika ni vyema Kushiriki katika Uchaguzi huo na kuendeleza Utulivu na Amani iliyopo.

Sauti ya Sheikh Mkuu wa Mkoa Wa Katavi akiwasisitiza Waisilamu kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu

kwa upande wao Wananchi wameeleza namna ambavyo walivyo upokea ujumbe huo kutoka kwa Sheikh  Mkuu wa Mkoa na kuahidi kwenda kutii na kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi ujao

Sauti za Wananchi Walioshiriki Swala ya Eid Al -Fitr wakieleza namna walivyomwelewa Sheikh Mkuu

Sikukuu ya Eid -Al -Fitr imesheherekewa April 10 Duniani kote na Waumini wa Dini ya Kiisilam ambapo Mkoani Katavi ilifanyika katika viunga vya Msikiti Mkuu wa Mkoa .