Mpanda FM

Ewura yaahidi huduma  bora  za maji ,umeme, petroli na gesi asilia

18 December 2023, 3:18 pm

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura imesema  inahakikisha mtumiaji anapata huduma  bora  za maji ,umeme, petroli na gesi asilia.

Na Lilian Vincent – KATAVI

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura imesema  moja ya jukumu lake ni kuhakikisha mtumiaji anapata huduma  bora  za maji ,umeme, petroli na gesi asilia.

Tobieta Makafu afisa uhusiano muandamizi mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji kanda ya magharibi  amesema mamlaka wamekuwa wakihusika kuweka viwango vya bei za maji,  masuala ya huduma ya umeme  pamoja na kuweka   bei za mafuta.

Sauti ya Tobieta Makafu

Kwa upande wake muhandisi na  Kaimu meneja  wa mamlaka hiyo kanda ya maghari walter christopher  amesema kwamba  moja ya jukumu lao ni kulinda maslahi ya watumiaji

Sauti ya Maghan Walter

Getrud  mbiling’i  afisa  muandamizi huduma kwa wateja   ameongeza kuwa  kama mamlaka wana jukumu pia la kutatua migororo ambayo inaweza kutokea baina ya mtumiaji na mhudumu.

Sauti ya Getrud Mbiling’i